Fahamu mifumo ya ulinzi ambayo Iran imetuma kwenda Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Droni aina ya Shahed-129 zikiwa katika maonyesho katika siku ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran

Taarifa iliyotolewa wiki iliyopita kuhusu jeshi la Iran kupeleka droni Urusi  haikuja kama jambo la kushangaza -taarifa kuhusu mipango ya Moscow ya kupata ndege zisizo na rubani (UAVs) kutoka kwa Tehran zilichapishwa mapema mwezi Julai, kulingana na uchambuzi wa mwandishi wa BBC Pavel Aksyonov.

Gazeti la  Marekani Washington Post liliandika katika majaribio ya kwanza ya droni ambazo Urusi ilikuwa tayari imezipata kutoka kwa Iran.

Jeshi la Urusi lina zaa nyingi za kijeshi ambazo kwa sasa hazifanyi kazi. Hatahibyo taarifa kuhusu ni zana zipi hazitolewi. 

Ingawa mpango wa ndege  zisizokuwa na rubani za Iran umekuwa ukiandaliwa tangu  mwishoni mwa mwa miaka ya 1980, nchi inakabiliwa na vikwazo, na wataalamu wanasema droni nyingi za Iran zimetengenezwa kwa kunakili miundo ya droni za kigeni.

 Ikikabiliwa na ukosefu wa droni wakati wa vita vya Ukraine,  Urusi ililazimika kuelekea Iran kwasababu kulikuwa na fursa chache za kununua aina hizo za silaha kutoka nchi nyingine na uzalishaji wa ndani ulikuwa wa kiwango cha chini, uchambuzi ulisema. 

Droni za Iran   

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Droni au ndege zisizokuwa na rubani za Iran  "Mohajer-6" katika  maonyesho ya kijeshi  Moscow  

Licha ya masharti ya kupata teknolojia ya kigeni, Iran inafahamika kama mtenezaji wa droni. Nchi hii imekuwa chini ya vikwazo vya kimataifa kwa na imepitia uzoefu wa   kuishi katika hali ngumu. 

 "Iran imekuw aikitengeneza ndege zisizokuwa na rubani tangu miaka ya 80 na imekuwa ikizipatia umuhimu. Ndio maana ina aina mbali mbali za droni, zikiwe mo za kimkakati,  za utambuzi wa maeneo yanayolengwa na droni za mashambulio.

Iran ililazimika kuishi  chini ya vikwazo na kununua kila kitu inachohitaji kuimarisha sekta yake ya jeshi licha ya vikwazo vinavyoikabili.

 Nchini Iran, hazitengenezwi tu  UAVs, makombora ya masafa marefu ya ballistic na silaha nyingine kali kama vile  mradi wa nyuklia ambao unaendelea licha ya vikwazo vyote dhidi yake ,"mtaalamu wa kijeshi wa Israeli  David Gendelman aliiambia BBC.

 Iran haiwezi kubuni ndege ya kijeshi peke yake, lakini imejifunza kutathmini na kuiga kutengeneza nakala ya teknolojia ya kigeni wakati wa kipindi cha vikwazo, anasema mtaalamu.

 Kwa njia hiyo, Wairan walijifunza ubunifu wa ndege ya kijesi ya Marekani-  American Northrop F-5 na hata wakaweza kuanzisha ndege zo wenyewe.   

 Sekta ya Iran ina uzoefu mkubwa katika utengenezaji wa vipuli kwa ajili ya ndege za kijeshi, iliyorithi kutoka enzi ya Shah . Zaidi ya hayo, inaaminiwa kuwa Iran ilikwepa vikwazo na kununua vipuli mbalimbali na vitu vingine kutoka ng’ambo.   

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Droni za Shah -171" , "Shahed-191" ni aina ndogo zaidi  ya muundo huu   

Urusi itanunua  droni zipi ?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana kituo cha utafiti cha ndege zisizokuwa na rubani za  kijeshi cha chuo cha   Bard ,kufikia mwaka 2019, Iran daraja la 1, 2 na 3  la ndege hizo  179.  

 

Daraja la kwanza lilijumuisha droni za kimkakati, quadcopters na  aircraft, na daraja la pili  na la tatu lilijumuisha  droni za uzani wa kati na nzito ( UAVs ) ambazo zimewekwa katika  kitengo cha  "masafa marefu"  kulingana na  kimo chake  (MALE UAV na  HALE UAV).

 Droni aina ya "Mohajer-6" iliyotolewa kwa Urusi iko katika daraja la pili kulingana na uainishaji huu . Kulingana na taasisi ya  Globalsecurity.Org, Irani ilizitumia katika nchi ya Afghanstan  miaka ya 1990.

 Licha ya jina lake linalofahamika sana, "Shahed-129" na "Shahed-191" ndege hizi zisizokuwa na rubani ni tofauti na  UAVs. Labda ni kwasababu zile za Magharibi zinazofanana nazozilikuwa tofauti pia.  

 Inaaminiwa kwamba  "Shahed-129" zilibuniwa kwa misinhi ya  droni za Israeli aina ya Hermes 450 ambazo ziliangukia mikononi mwa wahandishi wa Iran . "Shahed-191" ilitengenezwa kwa msingi wa  droni za Marekani zinazofahamika kama    American Q-170 Sentinel.  

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Droni zailizotengenezwa na Urusi  "Orion" katika maonyesho ya kijeshi  ya "Army-2017"  

Shirika lisilo la kiserikali la Marekani la kupambana na nyuklia nchini Iran"United Against Nuclear Iran - UANI" katika ripoti yake  "Tisho la mpango wa droni wa Iran " inasema kuwa inatumia  droni za Mohajer na Shahed-129 katika nchi za  Iraq na Syria. Ilisema kuwa droni hizi hushambulia maeneo yaliyolenhwa ndani ya Syria.   

 Iwapo Urusi ina nia ya katika UAVs za Iran, sio "kwasababu droni zao ni bora duniani," kwasababu utengenezaji katika Urusi yenyewe ni  ni wa kiwango cha chini sana, yote kwa ubora na uwingi, anasema David Gendelman.

 Kampuni ya Kronstadt nchini Urusi hutengeneza droni za Orion za aina ya  MALE. Mwezi Disemba  2021,  iliripotiwa kwamba droni hizi hata zilishambulia maeneo ndani ya Syria. Droni hizi za UAVs  zinatengenezwa katika kiwanda cha Dubna, karibu na Moscow.

 Mpango wa Iran ulitengeneza droni za UAVs  kuanzia mwaka 1988, kulingana na uchagnanuzi wa BBC.