Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara akamatwa Kigali
Chanzo cha picha, Reuters
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Diane Rwigara, mama yake na dada yake, wamekamatwa tena kwenye mji mkuu Kigali.
Polisi wanasema kuwa kando na makosa ya ulaghai na kukwepa kulipa kodi, watatu hao walikuwa ni tisho kwa usalama wa nchi na wanazuia uchunguzi.
Watu hao walishikwa kutoka nyumbani kwao mwezi uliopita ambapo baadaye polisi walikiri kuwa walikuwa wamewakamata.
Baadaye waliachiliwa. Wiki iliyopia wafuasi wa upinzani walishtakiwa kwa kujaribu kupindua serikali ya Rwanda.
Habari kuu
Gumzo mitandaoni
Zinazovuma zaidi
Haipatikani tena
{{rankTranslation}}