Vita vya Afghanistan: Urusi imekanusha kulipa wanamgambo ili kuvamia vikosi vya Marekani

Muda wa kusoma: Dakika 2

Urusi imekanusha madai kwamba ilijitolea kutoa zawadi kwa wanamgambo wanaohusishwa na kundil la Taliban kuua vikosi vya Marekani na vingine katika muungano wa Nato nchini Afghanistan.

Gazeti la The New York Times na la Washington Post yalinukuu maafisa waliosema kuwa kitengo cha kijajusi cha Urusi kilichohusika na majaribio ya mauaji Ulaya mwaka jana kilikuwa kimejitolea kutoa zawadi.

Ubalozi wa Urusi nchini Marekani ulisema kwamba madai hayo yamepelekea wanadiplomasia kupokea vitisho.

Kundi la Taliban lilikanusha kwamba kulikuwa na makubaliano kama hayo na kitengo cha ujasusi cha Urusi.

Taarifa hizo zinawadia huku Marekani ikijaribu kufanya mazungumzo ya makubaliano ya amani kumaliza vita vya Afghanistan vilivyodumu kwa miaka 19.

Kulingana na gazeti la New York Times, Rais Donald Trump aliarifiwa kuhusu taarifa hizo mwezi Machi, lakini Ikulu ya Marekani imekanusha madai hayo.

"Sio raisi wala naibu wake hakuna aliyearifiwa kuhusu madai yanayosemekana kutekelezwa na urusi," Msemaji wa Ikulu Kayleigh McEnany amesema.

Hatahivyo, aliongeza, " hili sio kwa misingi ya madai yanayosemekana ila kwa ukosefu wa usahihi wa taarifa za gazeti la New York Times ambalo linaangazia taarifa ya uongo kuwa Rais Trump aliarifiwa kuhusu suala hilo."

Afisa ambaye hakutajwa aliyenukuliwa na gazeti la New York Times amesema idara ya ujasusi ya Marekani ilihitimisha miezi kadhaa iliyopita kwamba kitengo cha ujasusi cha Urusi kilikuwa kinatafuta kuyumbisha wapinzani wake kisiri kwa kujitolea kutoa zawadi kwa mashambulizi yatakayofanikiwa dhidi ya muungano wa vikosi vya Nato.

Wanamgambo wa Kiislamu au makundi ya uhalifu yalioaminiwa kuwa na uhisiano nao, inasemekana kwamba yalikuwa yamepokea pesa, gazeti hilo limesema.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, ubalozi wa Urusi nchini Marekani ulishtumu gazeti hilo kwa kueneza taarifa za uongo.

Maafisa walionukuliwa na gazeti la New York Times walisema kuwa Baraza la Usalama wa taifa Ikulu, lilikuwa linatafakari namna ya kujibu madai hayo ikiwemo kuiwekea Urusi vikwazo vikali.

Inasemekana kwamba kitengo cha ujasusi cha Urusi pia kilikuwa kimehusishwa na jaribio la kuumua aliyekuwa jasusi wa Urusi Sergei Skripal na binti yake Yulia kwa kutumia kemikali inayoharibu neva huko Salisbury, Uingereza, Machi 2018.

Pia unaweza kutazama:

Msemaji wa kundi la Taliban ametaja madai hayo kama yasiyokuwa na msing

"Malengo yetu na kufanya mauaji yalikuwa yanaendelea tangu miaka kadhaa iliyopita na tulifanya hivyo kwa kutumia raslimali zetu wenyewe," Zabihullah Mujahid ameliambia gazeti la New York Times.

Aliaongeza kwamba Taliban ilikuwa imeacha kuvamia Marekani na vikosi vya Nato baada ya kufikia makubaliano Februari ya kuondolewa kwa vikosi hivyo kwa awamu na kuondolewa kwa vikwazo.

Kwa upande wa Taliban kama malipo ya makubaliano hayo, imesema kwamba haiwezi kuruhusu makundi yenye msimamo mkali kuendesha shughuli zao katika maeneo wanayodhibiti.