Mazishi ya kitaifa ya Rais Idris Deby yafanyika N'jamena
Mazishi ya kitaifa ya rais wa Chad Idriss Déby Itno yanafanyika Ijumaa katika mji mkuu wan chi hiyo N'Djamena kabla ya kuzikwa katika mkoa wake.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Chanjo mpya ya Malaria yaonesha ufanisi mkubwa
Chanzo cha picha, SCIENCE PHOTO LIBRARY
Ufanisi wa chanjo mpya ya malaria iliyotengenezwa nchini Uingereza
umefikia kiwango cha asailimia 77 katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Matokeo ya awali ya
kipimo cha chanjo hiyo yanaonesha kuwa na ufanisi zaidi katika dozi mojaya
chanjo.
Chanjo hiyo mpya
ilifanyiwa majaribio kwa watoto wachanga 450 nchini Burkina Faso.
Kutakuwa sasa na
upimaji wa watu wengi zaidi utakaowahusisha watoto takriban 5,000 kote barani Afrika.
Mwandishi wa BBC
anasema malaria huwauwa zaidi ya 400,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa ni wakazi
wa maeneo ya kusini mwa jangwa la sahara.
Wakenya wavamia tena mtandao wa IMF wakiilaumu kuikopesha nchi yao
Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mara ya pili wiki hii,
mtandao wa kijamii wa shirika la fedha duniani IMF umejipata ukivamiwa na
ukosoaji kutoka kwa Wakenya,wanaolilaumu kwa kuendelea kuikopesha fedha nchi
yao.
Matangazo
mubashara ya ukurasa wa Facebook ya IMFyalijazwa na maoni ya Wakenya ambao
hawataki madeni Zaidi yatolewe kwa serikali, wengi wao wakisema pesa nyingi
zitafanyiwa ubadhilifu nana maafisa wa taifa lao.
Katika
maoni yao, baadhi walielezea hofu kuhusumadeni ya umma ambayo yamefikia hadi dola bilioni 70 mwishoni mwa mwaka 2020.
Matangazo hayo yaliongozwa na Kristalina
Georgieva MkurugenziMkuu wa IMF Alhamisi usiku yaliyomalizika baada ya dakika 23.
Kwa picha: Mazishi ya rais wa Chad katika Idris Deby
Mazishi
ya rais wa Chad idris Deby, aliyeuawa mapema wiki hii kutokanana majeraha
aliyoyapata wakati wa mapigano ya waasi yanafanyika Ijumaa.
Rais Deby, ambaye
aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 30, alifariki siku moja baada ya matiokeo ya uchaguzi kuonesha kuwa ndiye mshindi
ambapo alikuwa anapanga kurejea
tena madarakani kwa muhula wa sita.
Mwanae wa kiume Mahamat
Idriss Déby Itno, al maarufu Jeneral Kaka, ataongoza nchi kwa miezi 18 hadi
uchaguzi utakapofanyika.
Mazishi ya kitaifa ya hayati Deby yanafanyika katika mji mkuu N'Djamena.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa hayati Rais Idriss Deby
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jenerali Mahamat Déby Itno (katikati) akiwa na maafisa wa serikali katika mazishi ya baba yake
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) amewasili nchini kuhudhuria mazishi yahayati Deby
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Maafisa wa jeshi la Chad wanafuatilia shughuli ya mazishi katika eneo walilotengewa
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Watu wamekusanyika nje kufuatilia mazishi ya driss Deby
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waandishi wa habari walipiga picha mwili wa Idriss Deby wakati wa mazishi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais wa Niger (kushoto), na marais wenzake kutoka Ufaransa na his French na Mauritania wakikutana N'Djamena Alhamisi kujadili mipango ya mazishi
AU yalaani kurefushwa kwa muhula wa rais Somalia
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Muungano wa Afrika umezitaka pande zote husika na mzozo wa Somalia kufufua mazungumzo kutatua mzozo
Muungano wa Afrika umelaani kurefushwa kwa muhula wa rais wa
SomaliaMohamed Abdullahi Farmajo na unatuma mjumbe
maalumu Mogadishu kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.
Baraza la Amani na Usalama la Muungano wa
Afrika lilitoa tangazo lake baada ya saa kadhaa za mazungumzo ya faragha ambapo
uliamua kupatanisha mzozo huo.
Taarifa iliyotolewa
baada ya kikao hicho Alhamisi ilizitaka pande zpote husika nchini Somalia "kufufua
mara moja mazungumzo juu ya misingi ya makubaliano ya yaliyofikiwa Septemba 2020
".
Dkt. Agnes Kijazi: Kimbunga Jobo kinaweza kuathiri pwani ya bahari Hindi na Ziwa Victoria
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Munira Noor
Nafasi, BBC Swahili
Chanzo cha picha, UN
Maelezo ya picha, Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes
Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya
hewa Tanzania (TMA ) na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
Dkt. Agnes Kijazi anasema kuwa Kimbunga Jobo kwa sasa kipo kilomita 236 kutoka
kisiwa Cha mafia Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.
“Kimbuga hiki kwa sasa kipo
kilomita 236 kutoka mashariki mwa kisiwa cha mafia, na kwa mwenendo huu
kitaendelea kuja katika maeneo ya nchi yetu, mawingu yanaendelea kusogea.”
Dkt. Kijazi ameongeza pia kwamba kimbunga hiki kinaweza kufikia ziwa victoria, kwani dalili za mawingu
zimeanza kuonekana upande wa ziwa Victoria.
Kimbunga hiki kinatarajiwa
kufika maeneo ya nchi kavu au mwambao wa pwani ya bahari nchini Tanzania ,
kuanzia tarehe 25. Na maeneo yatakayo athiriwa ni Lindi, Mtwara, Pwani,Dar es
salaam Unguja na ziwa Victoria.
Kwa upande wa athari zitakazo
tarajiwa Dkt. Kijazi amesisitiza kuwa watu wanaofanya shughuli katika bahari
kama wavuvi wachukue tahadhari dhidi ya kimbunga hiko. lakini pia wakazi wa
Maeneo ya pwani ya bahari, kwasababu kunatarajiwa kuwa na mvua pamoja na upepo
mkali
“Athari ambazo zinatarajiwa ni
upepo mkali baharini pamoja na mawimbi makala, lakini pia kikitua nchi kavu
upepo mkali utakuwepo nchi kavu, mara nyingi vimbunga kuambata na mvua kubwa,
kwa hiyo mafuriko yanaweza kutokea “ anasema Dkt Kijazi.
Kwa mujibu wa mashirika ya
kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa
zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.
Utabiri ulionyesha kuwa kimbunga hicho
kilipiata Ushelisheli Aprili tarehe 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa
na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.
Bobi Wine atakiwa kulipa mamilioni ya fedha ili arudishiwe gali lake la kifahari linaloshikiliwa
Chanzo cha picha, Bobi Wine /Twitter
Mamlaka ya mapato
nchini Uganda (URA), imemtaka kiongozi wa upinzani na mgombea wa uchaguzi Robert
Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, kulipa
ushuru ya shilling za Uganda milioni 337
sawa na dola 166,700, ili arudishiwe gari lake la land Cruiser.
Taarifa ya uamuzi huo kwa kiongozi wachama
cha National Unity Platform (NUP) inakamilisha mchakato wa mamlaka ya forodha nchini humowa kutathmini thamani ya gari hilo linalozuia
risasi, ambalo awali lililipiwa ushuru mdogo kwa kulinganishwa na gari lingine
la kawaida.
Akijibu juu ya
hatua kuthamanishwa upya kwa gari lake kupitia ujumbe wake wa twitter,
Bobi Wine amelalamikia hatua hiyo.
‘’Baada ya majaribio kadhaadhidi ya maisha yangu, baadhi ya marafiki
zangu walinipatia gali linalozuia risasi. Mara ya kwanza mambo yote alikuwa
mazuri kwasababu halikwa kwa jina langu. Interpol, Idara ya
uchunguzi ya polisi na URA wote
walilichunguza na kuliidhinisha . Ushuru unayotozwa na URA tuliilipa. Mambo yalianza kugeuka wakati
walipogundua kuwa ni gari langu’’
amesema:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Nigeria yaimarisha usalama kwenye mpaka wake na Chad
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Chad wamekuwa sehemu ya vikosi vinavyokabiliana na ukosefu wa usalama Afrika Magharibi
Waziri wa ulinzi wa Nigeria Bashir Magashi amesema kuwa nchi yake
imeimarsha usalama kwenye mpaka wake na Chad baada ya kifo cha rais wan chi hiyo.
Waziri huyo amesema
kuwa Nigeria inakabiliana na uasi ndani ya mipaka yake na inatambua tisho la
vitisho kutoka nje ambavyo vinaweza kusababishwa na kuingia kwa wakimbizi.
Ni Wanaigeria
wanaoishi Chad tu ambao wataruhusiwa kuingia nchini , Shirika la Habari la Reuters
limeripoti.
Mipaka ya Nigeria na
Chad ipo katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi ambako wanamgambo wa
Boko Haram wamekuwa wakiendesha mashambulio hivi karibuni.
Chad inaonekana kama nchi muhimu katika juhudi za Umoja wa Mataifa za
kupambana na ukosefu wa usalama Magharibi mwa Afrika
Chad yajiandaa kwa mazishi ya Rais Deby huku viongozi wakiwasili
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais Deby aliuawa katika eneo la mapigano
Mazishi ya kitaifa ya rais wa Chad Idriss Déby
Itno yatafanyika Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo N'Djamena kabla ya kuzikwa
katika mkoa wake.
Aliuawa Jumatatu
katika eneo la mapigano dhidi ya wapiganaji wa Front for Change and Concord in Chad (Fact), kikindi
cha wanajshi kilichoundwa na maafisa wa kijeshi mwaka 2016.
Viongozi wa mataifa ya
Mali na Guinea wamewasili, na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia anawasili kuelekea mjini N'Djamena licha ya onyo kutoka kwa waasi
kwamba kiongozi huyo wa kigeni hapaswi kuhudhuria kwa sababu za kiusalama.
Baada ya kutolewa kwa heshima za kijeshi na hotuba
mbali mbali, sala itafanyika katika msikiti wa Grand Mosque uliopo N'Djamena.
Baadaye , mwili wa Bw Déby's
utasafirishwa kwa ndege hadi Amdjarass,
kijiji kidogo kilichopo karibu na mji anakotoka wa Berdoba, uliopo zaidi ya kilomita 1000 (maili
621) kutoka mji mkuu, karibu na mpaka wa Sudan.
Rais Déby alikuwa mtu
muhimu katika mkakati wa usalama katika kanda ya Sahel.
Baraza la kijeshi
linaloongozwa na mwanae, Jeneral Mahamat Idriss lilichukua madara baada ya kifo
chake naanaungwa mkono kwa kiasi kidogo na jeshi lakini anauungwa mkono na
mtawala wa Ufaransa.
Generali Déby, 37, amesema jeshi litafanya uchaguzi wa
kidemokrasia katika kipindi cha miezi 18 ijayo, lakini viongozi wa upinzani wamelaani
hatua yake ya kuchukua mamlaka na kuitaja kama mapinduzi na jenerali wa kijeshi
amesema maafisa wengi wanapinga uongozi wake wa mpito.
Ni mpango ambao pia
waasi waliupinga huku pia wakionya kuwa watasitisha kipindi kidogo
kilichokuwepo cha usitishaji mpigano.
Mgawanyiko ndani ya
jeshi na upinzani vinamaanisha kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa usalama huku kukiwa
piwa nma changamoto za kiuchumi wakati Chad inaingia katika kipindi cha mpito .
Hujambo na karibu tena kwa matangazo haya Mubashara ya leo Ijumaa tarahe 23.04.2021