Malkia alazwa kwenye chumba cha kifalme kabla ya mazishi ya faragha ya familia
Ibada katika uwanja wa Windsor Castle ilikuwa hafla ya mwisho ya umma kabla ya Malkia kuzikwa karibu na mumewe, Mtawala wa Edinburgh.
Moja kwa moja
Jeneza la Malkia likipita katika kumbukumbu za wazazi wake wote wawili
Msafara huo unapoelekea kwenye Mall, hupita sanamu ambazo zilizinduliwa
na Malkia kwa heshima ya wazazi wake wote wawili.
Mnara wa shaba kwa ajili ya babake Mfalme George VIuilizinduliwa mapema
katika utawala wake, mwaka wa 1955.
Karibu ni mnara mwingine wa shaba ambao uliwekwa mwaka 2009 kama kumkumbuka
Mama wa Malkia, aliyefariki mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 10.
Umati wa watu unatulia tena huku msafara unapopita
Sio kwa mara ya kwanza katika kipindi cha siku 10
zilizopita, baadhi ya mitaa yenye shughuli nyingi zaidi katika mji mkuu huo
imetulia huku watu waliokusanyika kutazama msafara huo wakitoa heshima zao kwa
marehemu Malkia Elizabeth II.
Kengele kubwa inapigwa kila baada ya sekunde 60 huku
msafara ukiendelea polepole katika mitaa ya London.
Familia ya Kifalme ikitoa heshima wakati wanapita katika makumbusho ya vita vya Cenotaph
Awali, Mfalme Charles, Mkuu wa Wales, na Mwana wa Kifalme
walipigwa picha wakitoa heshima walipokuwa wakipita katika makumbusho wa vita
vya Cenotaph huko Whitehall.
Cenotaph ni mahali ambapo Huduma ya Kitaifa ya Ukumbusho
hufanyika kila Novemba.
Mwanamfalme Harry hajavaa sare ya kijeshi katika hafla ya
mazishi kwani yeye sio mfalme anayefanya kazi.
Jeneza la Malkia linaelekea wapi?
Msafara huu mkubwa zaidi utaelekea Wellington Arch,
mojawapo ya eneo kubwa huko London.
Saa 13:00 za kuwasili kwa BST zimepangwa - na ramani yetu
hapa chini inaonyesha njia itakayotumika.
Wanajeshi na polisi watajipanga njiani - pamoja na umati
mkubwa wa watu.
Endelea kuwa nasi tunapokufahamisha kuhusu safari ya
Malkia katika tukio hili muhimu.
Shughuli ya mazishi imeaanza
Msafara
mwingine sasa umeanza - tunatarajia kitu kikubwa zaidi kuliko gwaride
lililoonekana hapo awali.
Kutakuwa na vikundi saba, kila kimoja kikijumuisha
wanajeshi.
Wakati huu, Malkia Camilla, na Catherine, Mwanamfalme wa
Wales, watafuata kwa gari moja kwa moja nyuma ya Mfalme na washiriki wengine
wakuu, ambao watatembea tena nyuma ya jeneza.
Gari la pili litamchukua Meghan, Duchess wa Sussex, na
Sophie, Countess wa Wessex.
Huku wanaojumuisha Polisi la Kifalme la Canada wanaongoza
maandamano mbele kabisa.
Jeneza la Malkia limezungukwa tena na wabebaji na
walinzi.
Wakati huo huo, viongozi wa dunia wanaelekea kwenye
tafrija iliyoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje James Cleverly.
Chanzo cha picha, b
Katika picha: Umati huko London unatazama na kusikiliza ibada
Watu
nje ya abbey wamekuwa wakifuatilia ibada ya mazishi.
Maelezo ya picha, Hili ilivyo kwenye huko Mall
Maelezo ya picha, Wengine wanatazama mazishi kupitia simu zao...
Maelezo ya picha, Wengine wamelia...
Maelezo ya picha, ...huku wengine wakitafakari uhalisia huo
Maelezo ya picha, ...au ulisikiliza huduma kupitia vipaza sauti
Maombi kwa ajili ya Malkia ya ''kujitolea kusiko na kifani''
Msimamizi wa Kundi la Makanisa Huru Helen Cameron anasifu ''kujitolea kwa wajibu'' kwa Malkia na ''huruma yake kwa raia wake’’.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki la Roma nchini Uingereza na
Wales, Kadinali Vincent Nichols, anatoa shukrani kwa ''miunganisho mingi ya
umoja na kusaidiana alikoendeleza’’.
Askofu Mkuu wa York Stephen Cottrell anatoa shukrani kwa ''kujitolea
bila kuyumba kwa Malkia kwa Injili’’.
Maombi ya kushukuru kwa hekima, bidii na huduma ya Malkia
Msururu wa viongozi wa kanisa sasa wanasali katika ibada.
Kiongozi mkuu wa Kanisa la Scotland, Msimamizi wa Mkutano
Mkuu wa Iain Greenshields, anaanza, akitoa shukrani kwa ''maisha marefu na
utawala’’ wa Malkia na ‘’zawadi zake za hekima, bidii na huduma’’.
Viongozi wa huduma ya upendo ni nadra – Welby
Justin Welby
anazungumza juu ya wito wa Kibiblia wa kutumikia badala ya kuhudumiwa.
‘’Watu
wa huduma ya upendo ni wachache katika nyanja yoyote ya maisha. Viongozi wa
huduma ya upendo bado ni wachache,’’ anasema.
‘’Lakini
katika hali zote wale wanaohudumu watapendwa na kukumbukwa wakati wale wanaongangania
mamlaka na mapendeleo wanasahauliwa.’’
Anaendelea
kwa kusema ‘’alikuwa mwenye furaha, alikuwepo kwa wengi, akigusa maisha ya
wengi.’’
‘’Tunaomba
hasa kwa ajili ya familia yake yote, kuomboleza kama kila familia kwenye
mazishi - ikiwa ni pamoja na familia nyingi duniani kote ambazo zimepoteza mtu
hivi karibuni - lakini katika kesi ya familia hii kufanya hivyo ni katika
kuangaziwa’’.
Anaakisi
taarifa ya Malkia wakati wa virusi vya corona ambayo ilimalizika na maneno ya
wimbo maarufu wa Vera Lynn: ‘’Tutakutana tena.’’
Askofu
Mkuu wa Canterbury anamalizia mahubiri yake kwa kusema ‘’sote tunaweza
kushiriki tumaini la Malkia ambalo katika maisha na kifo lilihamasisha uongozi
wake wa utumishi’’.
‘’Huduma katika maisha, matumaini katika kifo.
‘’Wote wanaofuata mfano wa Malkia, na msukumo wa imani na
imani kwa Mungu, wanaweza kusema naye: ‘’Tutakutana tena.’’
Askofu Mkuu wa Canterbury atoa mahubiri
Askofu
Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, ameanza mahubiri yake.
“Mfano
wa viongozi wengi ni kuinuliwa kimaisha na kusahaulika baada ya kifo,” anasema.
“Mfano
kwa wote wanaomtumikia Mungu - maarufu au wasiojulikana, wanaoheshimiwa au
kupuuzwa - ni kwamba kifo ni mlango wa utukufu”.
Anaendelea:
“Marehemu Malkia alitangaza katika sherehe yake ya kuzaliwa ya miaka 21 kwamba
maisha yake yote atajitolea kulitumikia taifa na Jumuiya ya Madola.
"Ni
mara chache sana ahadi kama hiyo imetekelezwa vizuri."
Viongozi
wachache wamepokea kumiminiwa kwa upendo ambao sisi tumeona tangu kifo cha
Malkia, anaongeza.
"Mfano
wa marehemu Mkuu hakuwekwa kwa nafasi yake au matarajio yake bali ni nani
alifuata.
"Najua Malkia anashiriki imani sawa katika Yesu
Kristo kama mama yake.’’
Ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth imeanza huko Westminster Abbey
Kiongozi
wa Westminster, David Hoyle, anaongoza mazishi.
Lakini
ni Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, ambaye atatoa mahubiri na pongezi -
wakati wa sherehe Malkia amekabidhiwa kwa Mungu.
Maombi
yatatoka kwa Askofu Mkuu wa York, Kardinali Askofu Mkuu wa Westminster,
Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland na Msimamizi wa Makanisa Huru.
Waziri
Mkuu Liz Truss na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland wamepangwa
kutoa masomo ya leo - kutoka kwa maandiko.
Na itakuwa kwa kiongozi wa Westminster kutamka baraka.
Wanajeshi wa Ukraine walidai kuwa wamevuka mto mwishoni mwa juma
Chanzo cha picha, TELEGRAM/A_SHTIRLITZ
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine walisema walikuwa wamevuka mto mwishoni mwa juma
Vikosi vya Ukraine vinasema kuwa vimedhibiti tena ukingo wa mashariki wa
Mto Oskil, unaoonekana kuwa eneo la vita na wanajeshi wa Urusi
kaskazini-mashariki mwa Ukraine.
Jeshi la Urusi limekaribia kuondolewa kabisa katika eneo la Kharkiv na
kiongozi wa eneo hilo alisema walengwa wafuatao watakuwa jirani ya Luhansk.
Rais Volodymyr Zelensky alisema mashambulizi yanayofuata yalikuwa yanapangwa.
Wakati huo huo, Urusi ilishutumiwa kulenga kinu cha nyuklia kusini.
Mwendesha mtambo wa nyuklia wa Ukraine Enerhoatom alisema roketi ilitua
mita 300 (1,000ft) kutoka kwa vinu vya nyuklia kwenye kinu cha pili kwa ukubwa
nchini humo katika mkoa wa Mykolayiv, na kuharibu majengo na kuzima sehemu ya
kituo cha umeme kwenye uwanja huo.
Shambulio hilo halijathibitishwa kivyake, ingawa kampuni ilichapisha
picha za mlipuko karibu na tovuti.
Kiwanda kikubwa zaidi cha nyuklia cha Ukraine - na Ulaya - huko
Zaporizhzhia kimekuwa kikiwaka moto mara kwa mara tangu kilipokaliwa na majeshi
ya Urusi mwanzoni mwa vita na Umoja wa Mataifa umetoa wito wa eneo hilo kutambuliwa
kuwa salama ili kukilinda.
Paul Pogba: Kaka wa kiungo wa Juventus Mathias anazuiliwa kwa madai ya njama ya ulaghai
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mathias Pogba, kulia, aliungana na kaka yake Paul uwanjani kusherehekea ushindi wa Ufaransa wa Kombe la Dunia 2018.
Mathias
Pogba amezuiliwa na kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi kuhusiana na njama ya
kutaka kumnyanganya pesa kaka yake, mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul.
Watu
wengine wanne pia wamewekwa chini ya uchunguzi rasmi juu ya madai hayo na shirika
la uhalifu, vyanzo vya mahakama viliambia mashirika ya habari ya Reuters na
Agence France-Presse.
Wakili
wa Mathias Pogba, Yassine Bouzrou, alisema mteja wake hana hatia.
Aliliambia
shirika la utangazaji la Ufaransa BFMTV: ‘’Tutapinga uamuzi huu.’’
Mathias
Pogba, 32, amekiri kuwa alikuwa nyuma ya video ambayo ilionekana mtandaoni
mwezi uliopita ikiahidi ‘’ufichuzi’’ kuhusu kiungo huyo wa kati wa Juventus
mwenye umri wa miaka 29.
Waendesha
mashtaka wa Ufaransa walifungua uchunguzi wa kimahakama mapema mwezi huu baada
ya mchezaji wa zamani wa Manchester United Paul kusema alikuwa analengwa na
unyanganyi na vitisho kutoka kwa genge lililopangwa.
Aliwasilisha
malalamishi kwa waendesha mashitaka wa Turin mnamo tarehe 16 Julai akidai
alikuwa mlengwa wa njama ya ulaghai ya euro 13m (£11.29m).
Mshindi
wa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa mwaka 2018, Pogba alihamia Juventus kwa
uhamisho wa bure msimu huu baada ya kuondoka Manchester United.
Mathias
Pogba pia ni mchezaji wa kulipwa ambaye amewahi kuchezea Guinea na alichezea
vilabu kote Ulaya vikiwemo Crewe, Wrexham, Crawley na Partick Thistle.
Brazili yapiga marufuku uuzaji wa iPhones bila adapta za umeme za USB
Chanzo cha picha, Getty Images
Brazil inasema kuwa inapiga marufuku uuzaji wa iPhones ambazo
hazijumuishi adapta ya umeme.
Katika taarifa siku ya Jumanne, Wizara ya Sheria na Usalama wa Umma ya
Brazili ilisema imeitoza faini kampuni ya Apple faini ya reais milioni 12.275
(£2.04m).
Shirika la wateja la Brazil Senacon lilisema uamuzi wa Apple wa
kutojumuisha adapta za umeme na iPhone mpya unawabagua watumiaji kwa kuuza ‘’bidhaa
isiyokamilika’’.
Kampuni hiyo iliiambia Reuters katika taarifa kwamba itafanya kazi na
mamlaka ya Brazil ‘’kusuluhisha wasiwasi wao,’’ lakini ikaongeza kuwa hapo
awali ilishinda maamuzi kadhaa ya mahakama nchini Brazil kuhusu suala hilo.
‘’Tuna uhakika kwamba wateja wetu wanafahamu chaguzi mbalimbali za kuchaji
na kuunganisha vifaa vyao,’’ Apple ilisema.
Faini na kupiga marufuku uuzaji wa iPhones bila adapta za umeme za USB
zilitangazwa siku moja kabla ya Apple kuonyesha bidhaa zao za iPhone 14, 14 Pro
na Apple Watch Ultra.
Shirika la ulinzi wa watumiaji la São Paulo liliitoza Apple faini ya £2m
mwaka jana, ikisema uuzaji wa iPhone 12 na kila modeli tangu wakati huo,
unakiuka sheria za watumiaji kwa sababu hazija na chaja.
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed Bin Salman hatarajiwa katika mazishi ya Malkia
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman hatarajiwi tena
kuhudhuria mazishi ya Malkia, chanzo cha Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza
kimesema.
Chanzo hicho kilichonukuliwa na Reuters, kilisema mabadiliko hayo
yalifanywa na Wasaudi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa uamuzi wa kumualika Mwanamfalme,
ambaye ndiye mtawala mkuu wa Saudi Arabia.
Mwanamfalme huyo anayejulikana kwa jina la ‘’MBS’’, ameshutumiwa na
idara za kijasusi za nchi za Magharibi kwa kuamuru kuuawa kwa mwandishi wa
habari wa Saudi Jamal Khashoggi mnamo 2018. Hata hivyo, anakanusha shtaka hilo.
Lakini ameonekana kama mtu wa kawaida katika nchi za Magharibi na
hajawahi kwenda Uingereza tangu mauaji ndani ya Ubalozi mdogo wa Saudia mjini
Istanbul, mwandishi wa usalama wa BBC Frank Gardner anasema.
Vyanzo vilivyo karibu na Ubalozi wa Saudia vilithibitisha hapo awali
kwamba Mwanamfalme huyo angezuru London wikendi hii.
Lakini Turki al-Faisal, mfalme mwingine mwandamizi wa Saudi, anatarajiwa
kuhudhuria mazishi badala yake, chanzo cha Ofisi ya Mambo ya Nje kilisema.
Mashirika ya haki za binadamu yalisema mwaliko huo kwa Mohammed Bin
Salman uliwakilisha kuficha rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Saudia.
Mwaliko kwa Uchina pia ulisababisha utata, kwa sababu ya jinsi ilivyochukulia
Waislamu wa Uyghurs huko Xinjiang.
Mwanamuziki maarufu wa pop wa Urusi Alla Pugacheva alaani vita vya Ukraine
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Putin akimsalimiana na Alla Pugacheva huko Kremlin mnamo Desemba 2014
Mmoja wa waimbaji maarufu wa Urusi, Alla Pugacheva, ametoa wito kwa
mamlaka ya Urusi kumtangaza ‘’wakala wa kigeni ‘’, kwa mshikamano na mumewe
anayepinga vita sana Maxim Galkin.
Nyota wa showbiz pia, aliitwa ‘’wakala wa kigeni’’ siku ya Ijumaa baada
ya kulaani mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine.
Kwenye mtandao wa kijamii Pugacheva alimwita mumewe ‘’mzalendo wa kweli
wa Urusi asiyelaghaiwa, ambaye anataka ... kumaliza tabia ya vijana wetu kufa
kwa malengo ya uwongo’’.
Amekuwa nyota mkubwa kwa miongo kadhaa.
Alisema ‘’malengo ya uwongo’’ ya Kremlin huko Ukraine ‘’yanafanya nchi
yetu kuwa isiyopendeza na maisha ya raia wetu kuwa magumu sana’’.
Galkin, mcheshi, mtangazaji wa TV na mwimbaji, alitaka ‘’mafanikio kwa
nchi yake, amani na uhuru wa kujieleza’’, aliongeza.
Afisa mkuu wa Afya wa China ataka wananchi wasigusane na wageni
Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa mkuu wa afya wa China amewaonya wenyeji dhidi ya kuwagusa wageni, siku moja baada ya China kurekodi maambukizi yake ya kwanza ya homa ya nyani.
Katika chapisho kwenye mtandao wa Weibo, mtaalam mkuu wa magonjwa katika Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha China (CDC) Wu Zunyou alishauri dhidi ya "kugusana ngozi kwa ngozi na wageni".
Chapisho hilo lilizua utata, na wengine wakitaja kama ubaguzi wa rangi.
Sehemu ya Maoni kwenye chapisho asili tangu wakati huo imezimwa kwenye jukwaa.
"Ili kuzuia uwezekano wa maambukizo ya homa ya nyani kama sehemu ya maisha yetu ya afya, inashauriwa 1) usigusane moja kwa moja na wageni kwa ngozi," alisema Bw Wu kwenye ukurasa wake wa Weibo Jumamosi.
Aidha, Bw Wu pia alitoa wito kwa wenyeji kuepuka kugusana ngozi kwa ngozi na wasafiri wa hivi majuzi ambao walikuwa wamerejea kutoka nje ya nchi katika muda wa wiki tatu zilizopita, na pamoja na wageni.
Alichapisha maoni hayo siku moja baada ya mji wa kusini-magharibi wa Chongqing kuripoti kisa cha kwanza cha homa ya nyani kutoka kwa mtu aliyewasili kutoka nje ya nchi. Haijabainika ikiwa mtu huyo alikuwa raia wa China au mgeni.
Chapisho hilo, ambalo lilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa juma, liliibua maoni muhimu sana.
"Huu ni ubaguzi wa rangi kiasi gani? Vipi kuhusu wale kama mimi ambao wamekuwa wakiishi China kwa karibu miaka kumi? Hatujaona familia zetu kwa miaka 3-4 kutokana na mipaka kufungwa," aliandika mtumiaji kwenye mtandao wa Weibo, ambaye. alionekana kuwa mgeni.
Uchina imeweka baadhi ya hatua kali zaidi za Covid ulimwenguni tangu kuanza kwa janga hilo, ambazo zimejumuisha kufungwa kwa haraka, kufungwa kwa mipaka, upimaji wa lazima na vizuizi vya kusafiri.
Virusi vya homa ya nyani ambavyo huambukizwa kwa kuwasiliana kwa karibu na watu walioambukizwa, wanyama au vitu vilivyoambukizwa, kwa kawaida husababisha dalili kama vile homa, maumivu ya kichwa na vipele.
Kumekuwa na kesi zaidi ya 60,000 zilizothibitishwa na baadhi ya nchi zisizo za ugonjwa zimeripoti vifo vyao vya kwanza vinavyohusiana na homa hiyo.
Ethan Nwaneri
mwenye umri wa miaka 15 amekua mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia
ya ligi ya Uingereza kwenye mchezo wa ushindi wa 3-0 wa Arsenal dhidi ya Brentford.
Kiungo
mshambuliaji wa Uingereza, ambaye alizaliwa Machi 2007, alichukua nafasi ya
Fabio Vieira kwa washika mitutu wa London dakika za lala salama kwenye Uwanja
wa Brentford Community.
Akiwa na umri wa
miaka 15 na siku 181, Nwaneri alishinda rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Harvey
Elliott.
Kiungo wa kati
wa Liverpool Elliott alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 30 alipoichezea Fulham
mnamo 2019.
Nwaneri
alichukua nafasi ya Vieira, ambaye alikuwa amefunga bao la tatu, baada ya
dakika 91 na sekunde mbili. Alihusika kwa dakika tatu na sekunde 42 kabla ya
mchezo kumalizika baada ya dakika 94 na sekunde 44.
Ndiye mchezaji
wa kwanza chini ya umri wa miaka 16 kucheza kwenye Premier League.
"Tuna
nafasi ya kuleta wachezaji wachanga," alisema meneja wa Arsenal Mikel
Arteta kabla ya mchezo.
"Sisi tuna
upungufu sana na fursa huja wakati masuala yanapotokea."
Nwaneri amecheza
mechi kadhaa akiwa na wachezaji wa chini ya miaka 18 wa Arsenal na aliichezea
England timu ya chini ya miaka-16 alipokuwa na umri wa miaka 14.
Nwaneri ni nani?
Nwaneri alizaliwa tarehe 21 Machi 2007 punde tu baada ya Uwanja wa Emirates, uwanja wa nyumbani ambao Arsenal walihamia baada ya kuondoka Highbury, ulifunguliwa mwaka 2006.Amevutia haraka wakati akiwa na The Gunners.Akiwa na umri wa miaka 14, aliweka alama yake ya kwanza kwa vijana wa chini ya miaka 18 kwa bao dhidi ya Reading na kufuatiwa na maonyesho kadhaa ya kuvutia macho.
Alitarajiwa kutumia msimu huu na Vijana wa U-18 lakini alipandishwa haraka hadi Vijana wa U-21.Mnamo tarehe 8 Agosti, alifunga katika ushindi wa 3-0 baada ya kuingia kama mbadala wa England katika mchezo wa Vijana wa U-17 dhidi ya Visiwa vya Faroe.
Majeraha ya nahodha Martin Odegaard na Oleksandr Zinchenko yalimfanya Arteta akose nafasi ya kiungo dhidi ya Brentford."Ilikuwa hisia safi," aliongeza kocha wa Arsenal alipoulizwa kuhusu wakati alipoamua kumtuma Nwaneri.
Mashabiki wa Arsenal sasa watakuwa na matumaini kwamba anaweza kuendeleza maendeleo yake na kufuata mastaa kama Emile Smith Rowe na Bukayo Saka ili kuwa nyota mchanga katika klabu hiyo.
Malkia Elizabeth II: Mazishi ya kitaifa kufanyika leo London
Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya siku kadhaa za kuaga, mwili wa marehemu Malkia
Elizabeth II utaanza safari yake ya mwisho baada ya saa chache kama sehemu ya
mazishi makubwa ya serikali.
Mwili utasafirishwa kwanza hadi Westminster Abbey kwa
ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kuelekea kasri la Windsor
kwa ibada ya ki familia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya
kibinafsi.
Itakuwa siku ya hisia mbalimbali ikiwemo huzuni kubwa,
Hali ambayo haijashuhudiwa tangu mazishi ya mwisho ya kitaifa, yale ya Winston
Churchill, karibu miaka 60 iliyopita.
Umbali mfupi, kutoka Westminster Abbey, milango itafunguliwa kwa wageni kuanza kuwasili kabla ya ibada ya kidini mapema leo.
Wakuu wa nchi kutoka kote ulimwenguni wamekuwa wakiwasili kuungana na washiriki wa familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.
Wanasiasa wakuu wa Uingereza na mawaziri wakuu wa zamani pia watakuwepo.
Wanachama wa familia za kifalme kutoka kote Ulaya, ambao wengi wao walikuwa ndugu wa damu wa Malkia wanatarajiwa - Mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde na Mfalme Felipe wa Uhispania na Malkia Letizia watakuwa huko.Pia viongozi mbalimbali kutoka Afrika tayari wamewasili.