Unafahamu nini kuhusu vito vya Afrika vilivyoporwa na wakoloni?
Wakati wa ukoloni Afrika, maelfu ya vitu vya thamani na vya maana kubwa kitamaduni vilitwaliwa na mataifa ya magharibi na sasa vinapatikana katika makumbusho Ulaya na Marekani.
Lakini sasa, Ufaransa imezindua ripoti ambayo inatoa wito kwa turathi hizo za Afrika zilizo kwenye makumbusho nchini humo kurejeshwa Afrika. Hii imejiri huku wasimamizi wa makumbusho mengine makuu Ulaya wakisema wako tayari kuirejeshea Nigeria baadhi ya vitu vya thamani vilivyo Ulaya, lakini kwa mkopo.
Unafahamu nini kuhusu mali ya Afrika iliyoporwa?
Swali 1/6
Jiwe la Rosetta ndio lilikuwa ufunguo wa nyaraka ya jadi Misri. lakini ni nani aliyeligundua jiwe hilo zito (750kg), lililopo sasa katika jumba la ukumbusho Uingereza mnamo 1799?
Swali 1/6
Historia inayokubalika ni kuwa wanajeshi wa Ufaransa waliligundua jiwe hilo walipochimba msingi wa ngome katika Nile Delta.
Swali 2/6
Vikosi vya Uingereza vilinyakua mali ya Ethiopia katika vita vya Maqdala mnamo 1868. Lakini walitumia ndovu wangapi kubebea mali hiyo?
Swali 2/6
Ndovu 15 na punda 200 walihitajika kusafirisha mali iliyoporwa Maqdala. Ni pamoja na taji la dhahabu, vikombe na nyaraka za jadi za kikristo ambazo bado zipo katika taasisi tofauti Uingereza.
Swali 3/6
Ni wanyama gani wa Tsavo huitwa 'wala mtu' au man-eaters?
Swali 3/6
Simba wawili wa Tsavo waliwaua wafanyakazi 140 waliokuwa wanajenga reli kutoka Mombasa hadi ziwa Victoria mnamo 1898-1899, kabla ya kupigwa risasi na mhandisi raia wa Uingereza.
Swali 4/6
Mchongo wa mawe wa mwewe wa Zimbabwe ndio nembo kuu ya nchi hiyo. Baada ya kuporwa na wakoloni, kutoka magofu ya mji wa kale. Ni ndege wangapi kati ya wanane waliorudishwa Zimbabwe?
Swali 4/6
Michongo saba ilikuwepo Zimbabwe kufikia 2003 kipande cha chini cha mchongo mmoja kiliporejeshwa na Ujerumani. Mchongo wa nane upo katika chumba cha kulala cha Cecil Rhodes, ambaye nyumba yake katika mji wa Cape Town Afrika Kusini, sasa ni jumba la ukumbusho.
Swali 5/6
Sanamu maarufu la kuchongwa Malkia Bangwa lilichukuliwa kutoka inayojulikana sasa kama Cameroon mwishoni mwa karne ya 19. Wakaazi waliliita sanamu hilo la mwanamke “njuindem”. Maana yake?
Swali 5/6
“Njuindem” inamaanisha “mwanamke wa Mungu” katika lugha ya watu wa Bangwa. Sasa linamilikiwa na wakfu wa Dapper mjini Paris, Ufaransa baada ya Musee Dapper kufungwa mwaka 2017.Bado haijulikani vipi ajenti wa ukoloni wa Ujerumani Gustav Conrau alivyolipata mnamo 1899.
Swali 6/6
Je shaba za Benin zimetengenezwa kwa nini?
Swali 6/6
Ilioporwa na jeshi la Uingereza 1897, Shaba za Benin zimeundwa kutokana na shaba nyeupe. Nyingi zimesalia katika majumba ya ukumbusho Uingereza, Ujerumani na Marekani.
Kwa hisani: Muundaji: William Muli, Msanifu mchoro: Millicent Wachira, mchora vibonzo: George Wafula, Utafiti na uandishi: Ashley Lime, Wasimamizi: Hugo Williams na Muthoni Muchiri.
Unafahamu nini kuhusu mali ya Afrika iliyoporwa?
Swali 1/6
Nchi: Misri
Jiwe la Rosetta ndio lilikuwa ufunguo wa nyaraka ya jadi Misri. lakini ni nani aliyeligundua jiwe hilo zito (750kg), lililopo sasa katika jumba la ukumbusho Uingereza mnamo 1799?
- 1. Mvuvi wa Misri
- 2. Wanaakiolojia Waingereza
- 3. Wanajeshi wa Ufaransa chini ya utawala wa Napoleon
Jibu sahihi
Historia inayokubalika ni kuwa wanajeshi wa Ufaransa waliligundua jiwe hilo walipochimba msingi wa ngome katika Nile Delta.
Swali 2/6
Nchi: Ethiopia
Vikosi vya Uingereza vilinyakua mali ya Ethiopia katika vita vya Maqdala mnamo 1868. Lakini walitumia ndovu wangapi kubebea mali hiyo?
- 1. 0
- 2. 15
- 3. 3
Jibu sahihi
Ndovu 15 na punda 200 walihitajika kusafirisha mali iliyoporwa Maqdala. Ni pamoja na taji la dhahabu, vikombe na nyaraka za jadi za kikristo ambazo bado zipo katika taasisi tofauti Uingereza.
Swali 3/6
Nchi: Kenya
Ni wanyama gani wa Tsavo huitwa 'wala mtu' au man-eaters?
- 1. Maafisa wafisadi Kenya
- 2. Wanawake wanaoolewa na waume wengi
- 3. Simba wala watu
Jibu sahihi
Simba wawili wa Tsavo waliwaua wafanyakazi 140 waliokuwa wanajenga reli kutoka Mombasa hadi ziwa Victoria mnamo 1898-1899, kabla ya kupigwa risasi na mhandisi raia wa Uingereza.
Swali 4/6
Nchi: Zimbabwe
Mchongo wa mawe wa mwewe wa Zimbabwe ndio nembo kuu ya nchi hiyo. Baada ya kuporwa na wakoloni, kutoka magofu ya mji wa kale. Ni ndege wangapi kati ya wanane waliorudishwa Zimbabwe?
- 1. 7
- 2. 0
- 3. 1
Jibu sahihi
Michongo saba ilikuwepo Zimbabwe kufikia 2003 kipande cha chini cha mchongo mmoja kiliporejeshwa na Ujerumani. Mchongo wa nane upo katika chumba cha kulala cha Cecil Rhodes, ambaye nyumba yake katika mji wa Cape Town Afrika Kusini, sasa ni jumba la ukumbusho.
Swali 5/6
Nchi: Cameroon
Sanamu maarufu la kuchongwa Malkia Bangwa lilichukuliwa kutoka inayojulikana sasa kama Cameroon mwishoni mwa karne ya 19. Wakaazi waliliita sanamu hilo la mwanamke “njuindem”. Maana yake?
- 1. Mwanamke wa Mungu
- 2. Shujaa mkubwa
- 3. Mama mwenye furaha
Jibu sahihi
“Njuindem” inamaanisha “mwanamke wa Mungu” katika lugha ya watu wa Bangwa. Sasa linamilikiwa na wakfu wa Dapper mjini Paris, Ufaransa baada ya Musee Dapper kufungwa mwaka 2017.Bado haijulikani vipi ajenti wa ukoloni wa Ujerumani Gustav Conrau alivyolipata mnamo 1899.
Swali 6/6
Nchi: Benin
Je shaba za Benin zimetengenezwa kwa nini?
- 1. Shaba nyeupe
- 2. Mawe
- 3. Shaba Nyeusi