Kwa Picha: Mauaji Las Vegas, Marekani

Zaidi ya watu 50 wameuawa na takriban 100 kujeruhiwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu mwenye silaha alikuwa ghorofa ya 32 ya hoteli, upande mwingine wa barabara lilikokuwa likifanyika tamasha la muziki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walioshuhudia walisema mamia ya risasi zilifyatuliwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walioshuhudia walise kuwa kulikuwa na ghasia wakati watu walijaribu kukimbia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu walitoroka eneo hilo kwa haraka wakati wa ufyatuaji huo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Polisi waliambia watu kutokakaribia ukanda wa Las Vegas

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ufyatuaji huo ulifanyika wakati wa siku ya tatu na ya mwisho ya tamasha la muziki wa Country

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Polisi wanasema mshukiwa mmoja, mkaazi alipigwa risasi na kuuliwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Polisi walisema wanamtafuta mtu ambaye alikuwa akisafiri na mshukiwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mitaa ilifungwa na polisi wakamsimamisha mwanamume huyu ambaye aliendesha gari katika barabara ya Tropicana