Picha: Waislamu walivyosherehekea Eid ul-Fitr duniani

Waislamu pande zote za dunia washerehekea siku kuu ya Eid kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maadhimisho ya siku kuu ya Eid yalianza Jumapili Misri na mataifa mengine ya Kiarabu, baada ya mwezi kuonekana rasmi. Hapa ni katika kijiji cha Dalgamon nchini Misri, kilomita 120 kaskazini mwa mji wa Cairo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Msichana huyu alijipamba vilivyo wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid katika mji wa Mosul. Ni miongoni mwa raia wa Mosul wanaosherehekea siku kuu Eid bila udhibiti wa kundi la Islamic state nchini Iraq baada ya miaka mingi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waumini hawa waliadhimisha siku kuu ya Eid katika msikiti maarufu wa Blue Mosque mjini Istanbul, Uturuki.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Syria Bashar al-Assad (wa pili kutoka kushoto), ambaye anaendelea kushikilia maamlaka baada ya miaka sita ya mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe, ashiriki maombi ya kuadhimisha siku kuu ya Eid katika mji wa Hama

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Akina mama na wasichana wa Kiislamu katika ibada ya Eid, Gaza, Palestina. Misri ilianza kupeleka mafuta ya kuendesha kituo cha kuzalisha umeme mjini Gaza wiki hii na kutatua mzozo wa malipo uliotishia kusambaratisha sherehe za Eid.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waislamu mjini Moscow Russia walishiriki maombi barabarani karibu na msikiti mkuu. Moscow haina maeneo ya kutosha ya ibada kwa Waislamu, ambao asilimia kubwa ni wahamiaji kutoka katikati mwa Asia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waislamu hawa mjini London waliadhimisha siku kuu ya Eid katika bustani ya Dulwich.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waislamu wa Misri waachilia puto hewani baada ya maombi mjini Cairo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nchini Marekani, Waislamu walikongamana katika uga wa Anaheim, California.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ufilipino wametangaza kusitisha mapigano kwa muda dhidi ya magaidi wa Islamic State katika mji wa kiislamu wa Marawi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waumini wa Kiislamu wapanga foleni ili kupata futari Mexico City.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Msichana aonyesha mapambo ya hena wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid Karachi, Pakistan.