Kwa Picha: Moto wa London

Moto mkubwa umeteketeza jengo refu la makazi kusini mwa London usiku wa kuamkia leo

Chanzo cha picha, AFP/Guilio Thubum

Maelezo ya picha, Moto mkubwa ulitokea kwenye jengo moja magharibi mwa London usiku wa kumkia leo. Moto katika jengo la Grenfeel tower uliripotiwa saa 00:54BST

Chanzo cha picha, Natalie Oxford/PA

Maelezo ya picha, Kulingana wale walioshuhudia moto huo ulionekana kuanzia neo moja la jengo kabla ya kusambaa kuenda jengo lote

Chanzo cha picha, Gurbuz Binici /Getty Images

Maelezo ya picha, Walioshuhudia wameelezea watu waliokuwa wakipiga nduru wengine wakiruka kutoka manyumbani mwao kutafuta usalama

Chanzo cha picha, Reuters/Toby Melville

Maelezo ya picha, Moto uliteketeza jengo hilo ukianzia ghorofa ya pili na kusambaa hadi sehemu ya juu kabisa ya jengo

Chanzo cha picha, Reuters/Toby Melville

Maelezo ya picha, Kilichosababisha moto huo bado hakijulikani

Chanzo cha picha, AFP/Natalie Oxford

Maelezo ya picha, "Kilikuwa ni kitu kutoka kwa filamu ya Hollywood," mmoja wa wakaazi wa jengo hilo aliiambia BBC

Chanzo cha picha, Reuters/Toby Melville

Maelezo ya picha, Wakati wazima moto wanajaribu kuzima moto, maswali yameibuka kuhusu kile kilisababisha moto huo na ni kwa nini ulisambaa kwa haraka sana

Chanzo cha picha, Reuters/Toby Melville

Maelezo ya picha, Meya wa London Sadiq Khan ametangaza moto huo kuwa mkasa mkubwa

Chanzo cha picha, getty/Leon Neal

Maelezo ya picha, Wale wanaoishi karibu na jengo hilo waliamkia moshi wakati zima mopto walijaribu kupambana na moto huo

Chanzo cha picha, Carl Court/Getty Images

Maelezo ya picha, Helikopta ikipita huku moshi ukitoka kwenye jengo lililoteketea