Kwa Picha: Kuvumisha mavazi ya stara Dar es Salaam

Siku chache tu kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baadhi ya Wanawake wa kiislam nchini Tanzania wameungana na kuaandaa tamasha maalum kuhamasisha ujasiriamali na uvaaji stara kwa njia za kisasa zaidi.

Maelezo ya picha, Siku chache tu kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baadhi ya Wanawake wa kiislam nchini Tanzania wameungana na kuaandaa tamasha maalum kuhamasisha ujasiriamali na uvaaji stara kwa njia za kisasa zaidi.
Maelezo ya picha, Tamasha hilo kwa jina Stara Fashion Week liliandaliwa City Garden, Dar es Salaam.
Maelezo ya picha, Tamasha hili lilitokana na nia ya kupinga dhana potofu kuwa watu ambao hujifunika mavazi ya stara katika harakati ya maisha ni watu ambao wako nyuma kimaisha.
Maelezo ya picha, Wanaovalia wanasema mavazi hayo ya stara yanampa mwanamke heshima na kumfanya apendeze zaidi.
Maelezo ya picha, Lengo jingine la tamasha pia ni kwa wanawake nchini Tanzania kujiwezesha wenyewe kwa wenyewe.
Maelezo ya picha, Kwa sasa, hata wanawake ambao si Waislamu hununua mavazi ya stara kutoka kwa wabunifu wa mavazi wa ndani ya Tanzania na hawaagizi kutoka nje kama zamani ilivyokuwa, hususan kutoka nchi za Kiarabu.
Maelezo ya picha, Tamasha hufanyika kila mwaka. Hii ni mara ya tatu kwa maonesho hayo kufanyika.
Maelezo ya picha, Kupitia maonesho hayo, wanawake wanaofanya shughuli za kawaida kama vile kuuza ubuyu na pilipili wamehamasishwa kutangaza biashara zao kwa njia za kisasa, mfano kwa kutumia mitandao ya kijamii.