Kwa Picha: Maisha ya Fidel Castro

Picha za maisha ya Amri jeshi mkuu Fidel Castro,aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti na kuiongoza Cuba kwa miaka 50

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Fidel Castro alizaliwa mwaka wa 1926, mkoa wa kaskazini mashariki wa oriente nchini Cuba na tajiri wa ukuzaji wa miwa. Alijiunga na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Baada ya miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi yaliyotibuka, alienda mafichoni nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi kikaongoza. Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe 1, mwaka 1959, kama waziri mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mwaka 1961, Castro aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya wapiganaji raia wa Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni waliokuwa wanafadhiliwa na CIA na waliovamia Bay of Pigs kupigana dhidi ya serikali yake. Aliwashinda.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Alipata majaribio kubwa mwaka 1962, pale rais wa Marekani John Kennedy alipoionya Urusi kuondoa makombora yake kutoka Cuba.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwishowe, viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa besiboli. Hapa anaonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa 1962.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya raia wa Cuba walimchukulia kama dikteta kwa kuwakandamiza wapinzani.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao ,kuelekea Marekani, kwa kutumia maboti yaliyokuwa hatari.

Chanzo cha picha, OTHER

Maelezo ya picha, Lakini Fidel Castro alipata uungwaji mkono, na kuwa miongoni mwa viongozi waliohudumu kwa miaka mingi duniani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya urais kakake Raul. Alioneka mara chache hadharani, kabla ya kung’atuka madarakani mwezi Februari mwaka 2008.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwezi Septemba mwaka 2015, Fidel Castrol alihutubia umma kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne. Hotuba yake ilikuwa ya kwanza tangu mwezi Julai mwaka 2010 alipotoka kufanyiwa upasuaji wa utumbo. Alionekana kwa umma alipokuwa akisherehekea mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwake mwezi Agosti.