Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel

Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao baada ya moto mkubwa kuendelea kuenea na kukaribia kufika katika mji wa Haifa, kaskazini mwa nchi hiyo.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Moto mkubwa ambao umekuwa ukiwaka kwa siku kadha Israel sasa unakaribia mji wa Haifa kaskazini mwa nchi hiyo. Moto huo umesababisha uharibifu mkubwa. Watu karibu 50,000 katika mitaa minane wametakiwa kuhama, maafisa wanasema.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Hakujaripotiwa taarifa zozote za watu kuumia vibaya lakini watu kadha wamepelekwa hospitalini wakikabiliwa na matatizo kutokana na kupumua hewa iliyojaa moshi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ukosefu wa unyevu kwenye hewa pamoja na kuwepo kwa upepo mkali kumesababisha moto huo kuenea upesi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ndege iliyobebea maji ya kuzima moto ilipaa juu ya mji huo. Polisi wanasema wakazi wamekabiliwa na moto kutoka maeneo manne.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Katika baadhi ya maeneo ya Haifa, moto huo umeanza kukaribia sana majumba ya makazi.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Maeneo yanayokabiliwa na moto huo yalikuwa yamekabiliwa na kiangazi kwa miezi miwili. Mawaziri wanasema huenda moto huo uliwashwa makusudi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Moto huo hapa unaonekana ukiwaka karibu na barabara kuu ya Route 1 inayounganisha Tel Aviv na Jerusalem.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Maelfu ya wakazi wamehama makwao Haifa, wakijaribu kunusuru mali yao.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Wazimamoto wanaendelea na juhudi za kukabiliana na moto huo, ingawa umeathiri maeneo makubwa na wazimamoto hao ni wachache. Wanahitajika pia kuwalinda raia na nyumba zisishike moto.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Moshi kutoka kwa moto huo Haifa wakati mwingine ulikuwa mwingi kiasi kwamba karibu jua lizibwe.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Misitu iliyo karibu na Jerusalem pia inatishiwa. Israel imepokea usaidizi kutoka Urusi, Uturuki, Ugiriki, Italia, Croatia na Cyprus.