Kwa Picha: Maafa ya Kimbunga Matthew Haiti

Kimbunga Matthew ndicho hatari sana kutokea katika miaka ya hivi karibuni, kilisababisha mvua kubwa nchini Jamaica na visiwa vingine vya Caribbean.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kimbunga Matthew - Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba visiwa vya Caribean kwa kipindi cha miongo miwili - kimesababisha upepo mkali, mvua na dhoruba Haiti.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Serikali imejenga makazi 1,000 - kuwasitiri watu 340,000.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Saa chache kabla ya kuwasili kwa kimbunga Matthew, raia wa Haiti walitakiwa kuondoka nyumbani mwao.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Raia wengine walikataa kuondoka, wakiogopa mali yao kuibwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata familia zinazoishi kando ya mto zilikuwa zikikataa kuondoka

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kimbunga hicho kilitabiriwa kwamba kingesababisha upepo unaovuma kwa kasi ya 230km/h na kusababisha mvua ya kiwango cha inchi 40.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Haiti inashuhudia na viwango vya juu vya umaskini na majanga. Hili ni jiji kuu, Port-au-Prince.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Majengo hayajaafikia viwango vinavyohitajika vya ujenzi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raia katika maeneo yaliyofurika wakiokoa mali yao.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Nchini Jamaica, wamiliki wa maduka walifunga maeneo yao ya kazi kabla ya kuwasili kwa kimbunga hicho.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu waliookolewa kutoka nyumbani mwao mjini Kingston walipewa hifadhi kwenye uwanja wa michezo.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Selfie na Kimbunga Mathew viungani mwa Kingston.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Raia wa Cuba wajiandaa kabla ya kimbunga Mathew kuwasili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa kwenye hifadhi mjini Guantanamo, Cuba, kabla ya kuwasili kwa kimbunga Matthew.