Kwa Picha: Mfalme Akihito wa Japan

Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka. Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.

Chanzo cha picha, NHK

Maelezo ya picha, Kwenye hotuba yake ya pili kabisa kupitia runinga, Mfalme Akihito ameambia taifa hilo kuhusu changamoto za kuendelea na majukumu yake huku akitatizwa na umri na afya.

Chanzo cha picha, Kyodo

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito alitawazwa 1990, baada ya kifo cha babake, Hirohito, mwaka uliotangulia.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito alimuoa Malkia Michiko, raia wa kawaida, mwaka 1959. Walikutana wakicheza tenisi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akihito amekumbatia maisha ya kisasa tangu aingie madarakani, na kuipeleka familia ya kifalme karibu na wananchi.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kihistoria, mfalme alitazamwa kama 'miungu'. Hata hivyo, majukumu yake yalibadilishwa na kuwa 'ishara ya taifa' kwenye katiba mpya iliyoandikwa baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na nchi za Muungano baada ya Japa kushindwa vitani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito mara kwa mara ameeleza masikitiko yake kutokana na vitendo vya Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, jambo lililomfanya kutofautiana na viongozi kadha waliotaka kubadilisha mwenendo wa taifa hilo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwaka 2011, Mfalme Akihito na Malkia Michiko walisifiwa kwa kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga na tetemeko la ardhi. Mfalme Akihito pia alitoa hotuba yake ya kwanza kwa umma kupitia video.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mfalme an Malkia wamesimamia kipindi cha mabadiliko makubwa Japan na kuwa karibu zaidi na raia. Maelfu ya watu hufika kila mwaka mpya makao makuu ya kifalme kuwatakia heri.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Taarifa zilizotokea Julai kwamba Mfalme Akihito huenda angeng'atuka, jambo ambalo halijawahi kufanyika Japan, zilishangaza wengi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Lakini katiba inamzuia kuingilia siasa za nchi hiyo, na kunahitajika mabadiliko kwenye sheria za nchi hiyo ili kumruhusu kung'atuka.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito , ambaye ametatizwa na afya yake miaka ya karibuni, anataka kukabidhi baadhi ya majukumu kwa watu wengine wa familia yake.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mwishowe, mrithi wake atakuwa Mwanamfalme Naruhito, anayeonekana hapa upande wake wa kulia.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kupitia hotuba ya video ya dakika 10, ambayo ilirekodiwa awali, Mfalme Akihito amesema anatumai majukumu ya mfalme kama ishara ya taifa yataendelea bila matatizo.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Akihito ndiye Mfalme wa 125 katika familia ya kifalme ambayo inaaminika kutawala tangu karne ya tano, jambo linaloifanya kuwa familia ya kifalme ya kale zaidi duniani.