Tetesi za soka Ulaya: Arsenal, City, United na Chelsea zamgombea Anderson

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, 23, huku Manchester City, Manchester United na Chelsea pia wakimuwania (CaughtOffside).
Manchester United wanamfuatilia kiungo wa England, Adam Wharton, 22, ambaye yuko tayari kuondoka Crystal Palace ili kujiunga na klabu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (Sun).
Brighton wamelegeza msimamo wao kuhusu kumuuza kiungo wa Cameroon, Carlos Baleba, 22, na wanaweza kukubali dau la chini ya pauni milioni 100 walizotaka hapo awali (Sun).
Manchester United na Liverpool wanamtaka kiungo wa Ufaransa na Real Madrid, Aurelien Tchouameni, 26 (Fichajes).
Liverpool na Arsenal wamegonga mwamba katika jitihada zao za kumsajili winga wa Paris St-Germain na Georgia, Khvicha Kvaratskhelia, 25 (Teamtalk).
Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Hispania, Ferran Torres, 26, kutoka Barcelona msimu huu wa joto (Teamtalk).

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski, 37, kwa uhamisho wa bure iwapo ataondoka Barcelona (La Gazzetta dello Sport).
Juventus pia wanamuwania mshambuliaji wa zamani wa England, Mason Greenwood, 24, lakini Atletico Madrid nao wanapambana kumsajili kutoka Marseille (La Gazzetta dello Sport).
Kocha wa Hispania, Luis Enrique, 55, anatarajiwa kukataa kujiunga na Manchester United na badala yake atasaini mkataba mpya kubaki Paris St-Germain (i Paper).
Tottenham wanaweza kumgeukia Sean Dyche, 54, kuisaidia timu kuepuka kushuka daraja iwapo Roberto de Zerbi, 46, atasalia na msimamo wa kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu (Telegraph).
Everton wanapanga kumpa kocha wao David Moyes, 62, mkataba mpya kutokana na mafanikio ya kuibadilisha timu kutoka timu inayopambana kushuka daraja hadi kuwania nafasi za kucheza michuano ya Ulaya (Guardian).













