Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mahakama yatupilia mbali kesi ya kupinga uhalali wa Museveni kugombea tena urais

Mhakama ya Haki ya Afrika Mashariki imetupilia mbali kesi inayopinga uhalali wa Yoweri Museveni kugombea tena urais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. 'Mchungaji alikuwa na wasiwasi kutufungisha ndoa atapata dhambi'

    Nchini Tanzania, jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa upande wa serikali na hata mashirika yasiyo ya kiserikali ili kukabiliana na unyanyapaa uliopo dhidi ya watu wenye ulemavu. Hata hivyo, baadhi ya walemavu wanasema, changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni katika kutafuta wachumba, hali iliyomfanya Nyange Bobo ambae ni mlemavu wa viungo kuamua kuoana na mlemavu mwenzake Bi.Pauleta Mbisho.

  3. London Marathon 2020: 'Tunaweza kuleta tena matumaini duniani'

    Bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Mkenya Eliud Kipchoge anasema mbio za London Marathon mwaka huu "zinaweza kuleta matumaini duniani".

    Watu wengi watafuatilia mbio hizo kwa njia ya kidijitali huku wanariadha watakaoshiriki mbio hizo pekee wakikusanyika uwanjani mjini London Jumapili hii.

    "Tunaweza kuleta matumaini duniani kwa kuonesha kuwa tunaweza kufanya mazoezi katika mazingira ya kujitenga na kushindana hadharani kwa uweledi mkubwa," alisema Kipchoge.

    Alipoulizwa ikiwa tahifadhi taji lake, Kipchoge alijibu: "Bila shaka najiamini. Niko tayari kukimbia."

    Kipchoge amekiri kutokuwepo maelfu ya washangiliaji wa mbio hizo ambao hukusnyika kando kando ya barabara "kutazifany ambio hizo kukosa msisimko" unaohusishwa na mashindano hayo.

    Kipchoge, sawa na wanariadha wengine alifanyiwa vipimo vya corona kabla ya kuanza safari ya kutoka Kenya na alipofika mjini London.

  4. Chama cha walimu Uganda 'chahoji marufuku ya usafiri kwa wanafunzi'

    Chama cha waalimu nchini Uganda kimehoji hatua yakupiga marufuku wanafunzi kutumia usafiri wa umma, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

    Hatua hiyo imechukuliwa katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona wanafunzi wanaporudi s.

    Shule zilifungwa tangu mwezi Machi lakini zinatarajiwa kufunguluwa tena oktoba tarehe 15 kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya mwisho katika shule za msingi, za upili na elimu ya juu.

    Muongozo huo mpya pia unazitaka shule katika maeneo ya mjini kuwapa wanafuzi mabasi maalum katika bara bara zitakazoamuliwa routes.

    Lakini Katibu Mkuu wa Chama cha Waalimu Filbert Baguma amenukuliwa na Observer akisema ni vigumu kutekeleza muongozo huo kwasababi usimamizi wa shule hauwezi kudhibiti mienendo ya wanafunzi.

  5. Nigeria yabuni kifaa cha 'kupima haraka' Covid-19

    Nigeria imetengeza kifaa ya kufanyia vipimo vya Covid-19 ambacho kina uwezo wa kutoa matokeo ya ukaguzi wa sampuli chini ya dakika 40 na ambayo inaweza kutumiwa n ahata watu wasiokuwa na ujuzi wa hali ya juu.

    Waziri wa afya Olurunimbe Mamora amesema inafanya kazi kwa harakana bei yake ni nafuu mara 10 zaidi ya vifaa vinavyotumika sasa kufanya uchunguzi.

    Kifaa hicho bado hakijaidhinishwa na mamlaka inayohusika lakini imetoa matumaini ya nchi hiyo kuongeza juhudi za upimaji.

    Mamlaka zinasema kifaa hicho kinachojulikana kama SARS-COV-2 Isothermal Molecular Assay, kilitengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Nigeria.

    Nigeria kufikia sasa imewafanyia vipimo vya corona watu 500,000 kati ya watu karibu milioni 200.

    Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 58,000 walioambukizwa virusi vya coronana zaidi ya vifo 1,000. Idadi ya maambukizi ya kila siku imepungua.

  6. Ni nani aliyeshinda mdahalo wa kwanza kati ya Trump na Biden?

    Ilitabiriwa kuwa lengo la Donald Trump wakati wa mjadala huo lilikuwa kumkera Joe Biden - na ndani ya dakika chache kuanza kwake, ikawa wazi alipanga kufanya hivyo kwa kumkatiza mara kwa mara makamu wa rais wa zamani.

  7. Guinea 'imefunga mipaka' na majirani zake kabla ya uchaguzi

    Guinea imefunga mipaka yake na Senegal na Guinea-Bissau kabla ya uchaguzi mkuu, afisa wa serikali amenukuliwa na shirika la habari la AFP.

    Afisa huyo alisema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sababu za kiusalama kwa mujibu wa shirika hilo.

    Waziri wa usalama wa ndani Guinea-Bissau, Botche Cande, amesema mpaka huo umefungwa tangu siku ya Jumapili lakini mwezake wa Guinea hajathibitisha hilo.

    Rais wa Guinea Alpha Condé anagombea muhula wa tatu madarakani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba tarehe 18, hatua ambayo imezua utata.

  8. Mahakama yatupilia mbali kesi ya kupinga uhalali wa Museveni kugombea tena urais

    Mhakama ya Haki ya Afrika Mashariki imetupilia mbali kesi inayopinga uhalali wa Yoweri Museveni kugombea tena urais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

    Wakili wa Uganda Male Mabirizi alikuwa amewasilisha shauri katika mahakama hiyo ya kikanda kupinga uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ya nchi hiyo kudumisha hatua ya kufanyia marekebisho kiifungu cha sharia kinachoangazia ukomo wa umri wa wagombea urais.

    Marekebisho hayo yaliondoa masharti ya kumtaka mtu yeyote aliye na azma ya kuwania kiti cha urais awe na umri wa kati ya miaka 35 na 75.

    Bw. Mabirizi pia alihoji mchakato uliyotumiwa na bunge kuidhinisha mswada wa marekebisho ya katiba mwaka 2017, hatua ambayo ilisababisha vurugu bungeni hadi kikosi maalum cha wanajeshi kupelekwa kudhibiti vurugu hizo.

    Mahakama hiyo ya kikanda iliyo na makao yake mjini Arusha Tanzania, imeamua kuwa mchakato uliyotumiwa kuidhinisha mswada huo haukukika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  9. Mahakama yasitisha mgomo katika hospitali kubwa zaidi Afrika Mashariki

    Mahakama ya wafanyakazi nchini Kenya imesitisha mgomo wa uliyoitishwa na wafanyakazi wa hospitali Kuu ya Kenyatta, KNH.

    Jaji Maureen Onyango ameagiza zaidi ya wafanyakazi 5,000 kurejea kazini wakisubiri kusikizwa kwa kesi.

    Muungano wa wafanyakazi unaowawakilisha wauguzi, madaktari na wafanyakazi wengine katika hospitali hiyo umeagizwa kufika mbele ya mahakama hiyo Oktoba tarehe 6.

    Wafanyakazi wanalalamikia kucheleweshwa kwa malipo yao ya mishahara na marupurupu yaliyoboreshwa.

  10. Tembo 30 wa Zimbabwe 'waliuawa na bakteria'

    Maafisa wa wanyamapori nchini Zimbabwe wanashuku ugonjwa wa bakteria unaofahamika kama haemorrhagic septicaemia ndio chanzo cha vifo vya zaidi ya tembo 30 mwisho wa mwezi Agosti.

    Sampuli zimetumwa ili kufanyiwa uchunguzi zaidi.

    Tembo hao walikutwa wamelala kifudifudi, hali ambayo wataalamu wanaashiria walikufa ghafla.

    Wasimamizi wa mbuga za wanyama hawaamini waliuawa na wawindaji haramu, kwa sababu hawakutolewa pembe zao.

  11. Karibu katika matangazo mubashara Jumatano 30.09.2020