Yafahamu maeneo 5 'matakatifu' ya kale zaidi duniani

Kuanzia mawe ya siri ya Mongolia hadi miji iliyoanzishwa kuheshimu wafu, maeneo ya kale matakatifu yalijengwa na watu kujaribu kuelezea maana ya maisha, kifo na dunia yanapatikana katika maeneo mbali mbali ya sayari dunia. 

Maana ya maisha ni siri ambayo tamaduni nyingi ziumekuwa zikihangaika kuijua katika miaka yote.

Siri hii imepelekea kubuniwa kwa sehemu takatifu, huku watu duniani wakijenga majengo ya kuvutia ya kuheshimu miungi yao, huku wengine wakiamini ukuu wa vitu asili, wakitafuta jinsi ya kuwa na mahusiano na misitu mitakatifu, milima mitakatifu na miamba mitakatifu.    

 Kuanzia kujengwa kwa  Stonehenge  katika  England hadi piramidi za Chichen Itza nchini Mexico,ustaarabu wa kale ulifikia kiwango cha kuweka  misimu ya kipupwe hadi kiangazi, kukusanyika kwa mababu au kuwepo kwa uhusiano baina ya binadamu hai na roho za wafu.

Mambo yote haya yana uhusiano wa ukweli kwamba watu wamekuwa wakitaka kutafuta ukweli kuhusu maisha, kifo na dunia.  

 Neno "utakatifu" bila shaka limepotoshwa. Lakini kutokana na upatikanaji wa intaneti, huwa tunasahau kwamba bado kuna kitu ambacho hakijulikani kuhusu dunia yetu. 

Hatuwezi kusahau kwamba bado kuna maeneo matakatifu na   maeneo tambarare .

Utakatifu unaweza kuwa  njia tu iliyopo kwenye mto au kutembea kwenye eneo la bustani, kutafuta sauti asilia za nyikani."  Rainier anasema. 

Uchochoro cha mifupa ya Nyangumi ,Urusi  

Kwenye kisiwa cha  Yttygran , aneo la mbali , kisiwa chenye upepo  kilichopo kwenye  Bahari ya Siberia  ya  Bering, zinapatikana mifupa iliyopangwa ya mbavu za nyangumi na  uti wa mgongo inayofahamika kama  "Uchochoro wa mifupa ya nyangumi’’.

Eneo hili ambalo ni njia yenye urefu wa mita 550, iliyopo kando ya bahari ni eneo la kuvutia sana, anasema Chris Rainier, mtafiti wa masuala ya historia ya binadamu 

 Majengo haya ya mifupa ya nyangumi yalijengwa na watu wa jamii ya  Yupik, na inakadiriwa kuwa yamekuweko kwa miaka  2,000 ," Wanasema wataalamu

 Nadharia ya Kiakiolojia inaelezea kuwa eneo hilo lilikuwa ni mahala ambapo watu walikuwa wakikutana.

Walijenga mifupa ya nyangumi na kuiwekea Ngozi saw ana ile ya ng’ombe au dubu, juu ya jengo ili kubuni ukumbi wa mkutano. Walitumia eneo hilo kufanya mikutano mitakatifu. Kile kilichobakia kwa sasa ni mifupa ya nyangumi."

Hegra, Saudi Arabia

Hegra ulikuwa ni mji wa pili wa watu wa jamii ya Nabataea , ambao walijenga mji wao maarufu wa , Petra, zaidi ya kilomita 500 kaskazini magharibi mwa  Jordan ya sasa. 

Ukiwa katika jimbo la AlUla  la  Saudi Arabia, mji huo wa kale wa mawe  (unaofahamika kwa Waislamu kama Al-Hijr na Mada'in Salih) ulijengwa tangu Karne ya 1 BC ( Kabla ya Kristo). Ni eneo la  kwanza la nchi hiyo la urithi  la Shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO, eneo ambalo lina makaburi yaliyohifadhiwa vyema  zaidi ya 100 yaliyomo katika mawe.  

"Haya ni maeneo ya makaburi ya wafalme, Malkia na waheshimiwa, sawa tu   Petra,"  anasema Rainier.

Mwamba wa kale uliochongwa kwa ustadi wa hali ya juu unapatikana eneo lote la Kusini magharibi mwa Marekani, ikiwa ni pamoja na Utah, New Mexico, Arizona, na Colorado. Ikijulikana kama miamba iliyopinda-petroglyphs, picha hizi – ambazo nyingi zilibuniwa na  tamaduni za  Fremont na Anasazi  - mara nyingi huonyesha maumbile ya binadamu, wanyama, silaha za kuwinda na alama za mikono.

Maeneo haya yanachukuliwa kama maeneo matakatifu na Wamarekani wazawa, ambao ndani yake wanaiona kama viunganishi vinavyowaunganisha na nyakati zilizopita na urithi wa utamaduni wao.

"Nikiishi katika Santa Fe, New Mexico, nimekuwa kila mara nikivutiwa na watu wa Mataifa ya kwanza," Rainier anasema.

"Picha hii ilichukuliwa katika  Utah. Alama hizi za mikoni zinadhaniwa kuwekwa miaka ipatayo 4,000, lakini iko katika hali ya maridadi.

Mawe ya kale ya kulungu, Mongolia

“Mongolia ni nchi ya ajabu yenye historia ya kuvutia na ya muda mrefu,” anasema  Rainier. "Kuna maeneo ya makaburi ya kale yaliyotawanyika katika maeno mbali mbali ya kaskazini mwa Mongolia.

Wakati unapovuka eneo lenye savana, utaona rundo kubwa la mawe.

Ndani ya maeneo haya ya kuzika walizikwa mashujaa wa vita walioheshimiwa zaidi. Katika makaburi hayo vimezikwa vitu kama mikuki, maboksi ya vipuri, na mali nyingine mbali mbali ambazo wapiganaji hao jasiri walizimiliki wakati wa uhai wao."

Jengo maarufu la hekalu ya Angkor Wat  

Jengo la maarufu la hekalu ya Angkor Wat ni mnara mkubwa zaidi wa kidini duniani. Linachukua  kilomita za eneo 400, nje kidogo ya Siem Reap. Hekalu hilo lililojengwa karibu karne ya 12 kama makao makuu ya Himaya ya  Khmer Empire,  ambalo ni urithi wa UNESCO kwa sasa, mwanzoni lilitumika kama hekalu la Hindu , lakini liligeuzwa kuwa hekalu la Budha mwishoni mwa karne na hivi sasa ni mojawapo ya maeneo ya hija ya Wabudha.

 Makasisi, watawa, Wakambodia na wageni wa Kibudha huja hapa kila siku  kufanya ibada na kutoa sadaka, huku wasafiri  mara kwa mara wakikusanyika kila asubuhi kutizama jua likiwasha mwangaza hekalu – uzoefu wa kiroho kwa wengi. 

Eneo la  Angkor  linajumuisha hekalu 70 na karibu majengo 1, 000 ,  na kuwapa wasafiri wanaokuja kulizulu mengi ya kujifunza na kugundua. Kuna sanabu zisizohesabika za  Budha, pamoja na sanamu na vinyago vinavyoelezea hadithi za Kibudha, ingawa kwa heshima ya sanamu za Wahindu na vinyago pia vimehifadhiwa .